Chapa za kimataifa zaonyesha picha ya sungura, mnyama anayewakilisha Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2023 ili kukumbatia soko la China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 11, 2023
Chapa za kimataifa zaonyesha picha ya sungura, mnyama anayewakilisha Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa 2023 ili kukumbatia soko la China
Picha hii iliyopigwa Januari 8, 2023 ikionyesha bidhaa maalum zenye sura mpya za chapa ya kimataifa kwa ajili ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa Sungura wa 2023 kwenye duka lisilotozwa ushuru huko Haikou, Mkoa wa Hainan, Kusini mwa China. Mwaka Mpya wa Jadi wa China unapokaribia, chapa za kimataifa zinatoa bidhaa maalum zenye sura mpya ili kukaribisha Mwaka wa Sungura na kukumbatia soko kubwa la China. Bidhaa nyingi maalum zimewekwa picha ya sungura, mmoja wa wanyama 12 wa Kalenda ya Kilimo ya China, na zingine zimewekwa rangi nyekundu ambayo ni rangi maalum na yenye kuashiria bahati nchini China. (Xinhua/Guo Cheng)
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha