Mapambo yenye picha ya sungura yaongeza shamrashamra za sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 17, 2023
Mapambo yenye picha ya sungura yaongeza shamrashamra za sherehe za Mwaka Mpya wa Jadi wa China
Mtu akinunua bidhaa za mapambo kwa ajili ya sherehe zijazo za Mwaka Mpya wa Jadi wa China katika duka moja lililopo Wilaya ya Longhui, Mji wa Shaoyang katika Mkoa wa Hunan wa China, Januari 16, 2023.

Mwaka Mpya wa Jadi wa China wa Sungura unapokaribia, mapambo na kazi mbalimbali za mikono zenye picha ya sungura, mmoja wa wanyama 12 ambao kila mmoja anawakilisha mwaka mmoja katika mzunguko wa miaka 12 kwa kalenda ya kilimo ya China, zimeteka mitaa mbalimbali, na kuongeza shamrashamra za sherehe hiyo maarufu ya kijadi nchini China. (Picha na Zeng Yong/Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha