Watu wa Kabila la Wamiao washiriki katika shughuli ya kucheza ngoma katika Mkoa wa Guizhou, China
 |
Watu wa kabila la Wamiao wanaovaa mavazi ya kijadi wakishiriki katika shughuli ya ngoma ya kitamaduni iitwayo "Tiaoyue" katika Kijiji cha Zhongpai, Wilaya ya Longli katika Mkoa wa Guizhou, Kusini-Magharibi mwa China, Januari 29, 2023. "Tiaoyue", maana yake ni kucheza ngoma chini ya mwanga wa mwezi, ikitokana na mila na desturi za Wamiao za kuombea Baraka na kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China, ambapo vijana huchukua fursa hii kuonyesha upendo na kupata wenzi watarajiwa. (Xinhua/Yang Wenbin) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)