Habari Picha: Mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Tanzania

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 01, 2023
Habari Picha: Mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Tanzania
Picha hii iliyopigwa Februari 23, 2023 ikionyesha mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar, Tanzania. Mji Mkongwe wa Zanzibar ulikuwa mji mkuu wa Dola ya Sultani ya Zanzibar. Ni eneo lenye kubeba mchanganyiko wa tamaduni mbalimbali za Afrika, Asia na Ulaya. Mnamo Mwaka 2000, mji huo wa kihistoria uliorodheshwa kuwa eneo la Urithi wa Utamaduni wa Dunia na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO). (Xinhua/Dong Jianghui)
(Wahariri wa tovuti:Shixi,Zhao Jian)

Picha