Wakulima huko Hangzhou waanza kuvuna majani ya chai ya Longjing kabla ya Siku ya Qingming
 |
Mkulima akikoroga na kukaanga majani ya chai ya Longjing katika Kijiji cha Longjing, huko Hangzhou, Mkoa wa Zhejiang, Mashariki mwa China, Machi 13, 2023.
Chai ya Longjing, inayojulikana pia kwa jina la chai ya China ya Ziwa Dragoni Magharibi, ina sifa ya rangi yake ya kijani kibichi, harufu nzuri, ladha laini na mwonekano mzuri.
Wakulima huko Hangzhou sasa wanaanza kuvuna majani ya chai ya Longjing kabla ya Siku ya Qingming ambayo ni siku ya jadi ya kusafisha makaburi nchini China, ili kuzalisha chai ya Mingqian (ikimaanisha "kabla ya Qingming"), ambayo hutengenezwa kwa majani chipukizi ya chai ya kwanza kabisa katika majira ya mchipuko na huchukuliwa kuwa yenye ubora wa juu. (Xinhua/Xu Yu) |
(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)