Maonyesho ya Kimataifa ya tasnia za Utamaduni yafunguliwa Shenzhen, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 08, 2023
Maonyesho ya Kimataifa ya tasnia za Utamaduni yafunguliwa Shenzhen, China
Sanaa za dragoni zikionekana kwenye banda la Maonyesho ya 19 ya Tasnia za Utamaduni ya Kimataifa ya China (Shenzhen) ambayo yamefunguliwa Juni 7 huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China China (People's Daily Online)

SHENZHEN - Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Tasnia za Utamaduni ya China (Shenzhen) yameanza siku ya Jumatano huko Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong Kusini mwa China, yakitarajiwa kuingiza msukumo mpya katika maendeleo ya tasnia ya utamaduni nchini China.

Maonyesho hayo ya siku tano, yanayohusisha shughuli za nje ya mtandao, yanavutia vyombo vya kiserikali, mashirika ya kitamaduni na kibiashara zaidi ya 3,500.

Eneo la maonyesho ya kidijitali la China limeanzishwa kwa mara ya kwanza ili kuangazia na kukuza wahusika wa soko la ngazi ya kitaifa, majukwaa makuu na matokeo ya uvumbuzi yenye teknolojia ya kisasa zaidi katika tasnia ya utamaduni.

Majukwaa, makongamano, shughuli za kutia saini mikataba, na mashindano ya ubunifu pia yatafanyika ili kushiriki habari na kuhimiza maendeleo ya uvumbuzi wa tasnia ya utamaduni.

Tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2004, maonyesho hayo ya utamaduni yameshuhudia upanuzi unaoendelea katika ukubwa wa eneo lake la maonyesho, idadi ya wageni na kiwango cha kuwa ya kimataifa. Yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza maendeleo na ufunguaji wa tasnia ya utamaduni ya China.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha