

Lugha Nyingine
Maonyesho ya Kimataifa ya tasnia za Utamaduni yafunguliwa Shenzhen, China
![]() |
Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Tasnia za Utamaduni ya China (Shenzhen) yamefunguliwa huko Shenzhen, Mkoa wa Guangdong, Kusini mwa China, Juni 7, 2023.(Tovuti ya Gazeti la Umma) |
SHENZHEN - Maonyesho ya 19 ya Kimataifa ya Tasnia za Utamaduni ya China (Shenzhen) yameanza siku ya Jumatano huko Shenzhen katika Mkoa wa Guangdong Kusini mwa China, yakitarajiwa kuingiza msukumo mpya katika maendeleo ya tasnia ya utamaduni nchini China.
Maonyesho hayo ya siku tano, yanayohusisha shughuli za nje ya mtandao, yanavutia vyombo vya kiserikali, mashirika ya kitamaduni na kibiashara zaidi ya 3,500.
Eneo la maonyesho ya kidijitali la China limeanzishwa kwa mara ya kwanza ili kuangazia na kukuza wahusika wa soko la ngazi ya kitaifa, majukwaa makuu na matokeo ya uvumbuzi yenye teknolojia ya kisasa zaidi katika tasnia ya utamaduni.
Majukwaa, makongamano, shughuli za kutia saini mikataba, na mashindano ya ubunifu pia yatafanyika ili kushiriki habari na kuhimiza maendeleo ya uvumbuzi wa tasnia ya utamaduni.
Tangu kuanzishwa kwake Mwaka 2004, maonyesho hayo ya utamaduni yameshuhudia upanuzi unaoendelea katika ukubwa wa eneo lake la maonyesho, idadi ya wageni na kiwango cha kuwa ya kimataifa. Yamekuwa jukwaa muhimu la kukuza maendeleo na ufunguaji wa tasnia ya utamaduni ya China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma