Siku ya tano ya Michezo ya Chengdu Universiade: Waogeleaji wa China wapata medali 4 za dhahabu (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 03, 2023
Siku ya tano ya Michezo ya Chengdu Universiade: Waogeleaji wa China wapata medali 4 za dhahabu
Qin Haiyang wa China akishiriki kwenye fainali ya kuogelea mita 100 kwa wanaume katika Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia (FISU) inayoendelea huko Chengdu, kusini-magharibi mwa Mkoa wa Sichuan wa China, Agosti 2, 2023. (Xinhua/Wu Gang)

Waogeleaji wa China walitawala mashindano ya kuogelea na kupata medali nne kati ya sita za dhahabu zilizogombewa jana kwenye Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia (FISU) inayoendelea huko Chengdu. Zhang Yufei kutoka Chuo Kikuu cha Kusini-mashariki cha China, mshindi wa mchezo wa kuogelea kwa mtindo wa kipepeo mita 200, na mshindi wa pili katika kwa mtindo huo mita 100 katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, alitumia muda wa sekunde 25.20, ambayo ni rekodi mpya kwenye michezo hiyo, na kunyakua medali ya dhahabu ya mchezo wa kuogelea mita 50 kwa mtindo wa kipepeo kwa wanawake.

Qin Haiyang, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tongji alishinda medali nne za dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya Aquatics yaliyomalizika hivi karibuni nchini Japan, alikuwa nafasi ya mbele kabisa katika mbio za mita 100 kwa wanaume baada ya kutumia muda wa sekunde 58.92.

Mashindano yote ya kuogelea yatakamilika Agosti 7, na medali 32 zaidi za dhahabu zitagombewa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha