

Lugha Nyingine
Siku ya tano ya Michezo ya Chengdu Universiade: Waogeleaji wa China wapata medali 4 za dhahabu (3)
![]() |
Liu Yaxin wa China akiwa kwenye fainali ya kuogelea mita 200 kurudi nyuma kwa wanawake kwenye Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia (FISU) inayondelea huko Chengdu, kusini-magharibi mwa Mkoa wa Sichuan wa China, Agosti 2, 2023. (Xinhua / Chen Zeguo) |
Waogeleaji wa China walitawala mashindano ya kuogelea na kupata medali nne kati ya sita za dhahabu zilizogombewa jana kwenye Michezo ya 31 ya Vyuo Vikuu ya Dunia (FISU) inayoendelea huko Chengdu. Zhang Yufei kutoka Chuo Kikuu cha Kusini-mashariki cha China, mshindi wa mchezo wa kuogelea kwa mtindo wa kipepeo mita 200, na mshindi wa pili katika kwa mtindo huo mita 100 katika Michezo ya Olimpiki ya Tokyo, alitumia muda wa sekunde 25.20, ambayo ni rekodi mpya kwenye michezo hiyo, na kunyakua medali ya dhahabu ya mchezo wa kuogelea mita 50 kwa mtindo wa kipepeo kwa wanawake.
Qin Haiyang, mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tongji alishinda medali nne za dhahabu katika Mashindano ya Dunia ya Aquatics yaliyomalizika hivi karibuni nchini Japan, alikuwa nafasi ya mbele kabisa katika mbio za mita 100 kwa wanaume baada ya kutumia muda wa sekunde 58.92.
Mashindano yote ya kuogelea yatakamilika Agosti 7, na medali 32 zaidi za dhahabu zitagombewa.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma