Wilaya ya Laishui ya Kaskazini mwa China yaimarisha kazi ya uokoaji baada ya kimbunga (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 09, 2023
Wilaya ya Laishui ya Kaskazini mwa China yaimarisha kazi ya uokoaji baada ya kimbunga
Picha hii inaonesha mfanyakazi anayeendesha kijiko cha kuondoa tope kwenye barabara katika Kijiji cha Xiazhuang cha Mji wa Sanpo wa Wilaya ya Laishui, Kaskazini mwa Mkoa wa Hebei China, Agosti 8, 2023.

Wilaya ya Laishui iliyoathiriwa na Kimbunga Doksuri, hivi karibuni ilikumbwa na mvua kubwa na baadhi ya vijiji vilikumbwa na matatizo ya usafiri na mawasiliano. Hivi sasa mamlaka za mitaa zinarekebisha miundombinu iliyoharibiwa na mafuriko ili kurejesha maisha katika hali ya kawaida haraka iwezekanavyo. (Xinhua/Yang Shiyao)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha