Katika picha: Eneo la urithi wa dunia la UNESCO, michoro kwenye miamba mkoani Guangxi, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2023
Katika picha: Eneo la urithi wa dunia la UNESCO, michoro kwenye miamba mkoani Guangxi, China
Zhu Qiuping, mtaalamu wa ulinzi wa mabaki ya utamaduni, akiangalia michoro kwenye miamba ya Huashan katika wilaya ya Ningming, mji wa Chongzuo, Mkoani Guangxi, China Agosti 8, 2023. (Xinhua/Zhang Ailin).

Michoro ya rangi hudhurungi, ilichorwa tangu wakati wa Madola ya Kivita (475-221 KK) hadi wakati wa enzi ya Han Mashariki (25-220), inaonyesha matambiko ya watu wa Luoyue, mababu wa kabila la wazhuang.

Inasemekana kuwa picha kuu za michoro hiyo ni watu wenye umbo la chura – alama ya kabila la wazhuang. Baadhi ya michoro hiyo pia inaonyesha matukio ya michezo.

Hadi sasa bado ni kitendawili kujua ni jinsi gani watu wa Luoyue waliweza kupaka rangi kwenye miamba hiyo. Kundi la michoro ya miamba liliwekwa kwenye orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO mwaka 2016. (Xinhua/Zhang Ailin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha