Katika picha: Eneo la urithi wa dunia la UNESCO, michoro kwenye miamba mkoani Guangxi, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 10, 2023
Katika picha: Eneo la urithi wa dunia la UNESCO, michoro kwenye miamba mkoani Guangxi, China
Picha hii iliyopigwa Agosti 8, 2023 inaonesha sehemu ya michoro iliyoko kwenye miamba ya Huashan katika wilaya ya Ningming, Chongzuo, Kusini mwa Mkoa wa Guangxi, China. Eneo la Zuojiang Huashan lina michoro zaidi ya 1,900 iliyohifadhiwa vizuri kwenye uso wa milima ya Huashan kando ya Mto Zuojiang na kijito cha Mingjiang huko Chongzuo.

Michoro ya rangi hudhurungi, ilichorwa tangu wakati wa Madola ya Kivita (475-221 KK) hadi wakati wa enzi ya Han Mashariki (25-220), inaonyesha matambiko ya watu wa Luoyue, mababu wa kabila la wazhuang.

Inasemekana kuwa picha kuu za michoro hiyo ni watu wenye umbo la chura – alama ya kabila la wazhuang. Baadhi ya michoro hiyo pia inaonyesha matukio ya michezo.

Hadi sasa bado ni kitendawili kujua ni jinsi gani watu wa Luoyue waliweza kupaka rangi kwenye miamba hiyo. Kundi la michoro ya miamba liliwekwa kwenye orodha ya urithi wa dunia ya UNESCO mwaka 2016. (Xinhua/Zhang Ailin)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha