Wanakijiji walioathiriwa na mafuriko warudi nyumbani katika Mji wa Tianjin, China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 18, 2023
Wanakijiji walioathiriwa na mafuriko warudi nyumbani katika Mji wa Tianjin, China
Wanakijiji wakirudi nyumbani katika Kijiji cha Shaoqidi kilichoko Kitongoji cha Huanghuadian, Wilaya ya Wuqing katika Mji wa Tianjin, Kaskazini mwa China, Agosti 17, 2023. (Xinhua/Sun Fanyue)

Jumla ya watu 15,011, kundi la mwisho la wale ambao hapo awali walihamishwa kutoka maeneo hatari kwa mafuriko kando ya Mto Yongding wamerejea majumbani mwao kwenye vijiji 14 vya Wilaya ya Wuqing katika Mji wa Tianjin, China siku ya Alhamisi. Kwa sasa, utoaji wa umeme, maji, na gesi umerejeshwa katika vijiji hivyo, na tathmini na ukarabati wa vifaa vilivyoharibiwa unaendelea katika maeneo husika.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha