Waandishi wa habari wa nchi za Eurasia wasifu uchumi wa Kidijitali wa Guizhou

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 30, 2023

“Hapa China, nimeona manufaa makubwa kwa maisha ya watu yanayoletwa na uchumi wa kidijitali, na matumizi ya hali mbalimbali yanastahiki kuigwa na nchi yangu." Oktoba 27, ujumbe wa vyombo vya habari vya Eurasia uliotembelea Guizhou ulifika kwenye Kituo cha kitaifa cha kufanya mawasiliano na kujihisi cha eneo la majaribio ya jumla ya Data Kubwa. Baada ya kutazama hali mbalimbali ya matumizi ya Data kubwa, Meneja wa Biashara wa Gazeti la Maoni la Kyrgyzstan(Slovo Kyrgyzstana)Bw. Umatkul Bralkieva alisifu sana aliyoshuhudia .”

Mwaka huu ni maadhimisho ya miaka kumi tangu kutolewa kwa pendekezo la kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Ili kuimarisha mawasiliano kati ya vyombo vya habari vya nchi washirika wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kusaidia watu nchi hizo , hasa vijana wao kuelewa maana ya Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na kushuhudia mafanikio mengi ya Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" , Tovuti ya Gazati la Umma(People's Daily Online) imeanzisha mradi wa Mawasiliano ya kirafiki wa Vijana wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Hivi sasa shughuli ya mradi huo ya Vyombo vya habari vya nchi za Eurasia kutazama Guizhou ilianzishwa rasmi katika Mji wa Guiyang, China.

Waandishi wa habari wakitembelea kwenye bustani ya Guanshanhu. (Picha na Ynagqian/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Waandishi wa habari wakitembelea kwenye bustani ya Guanshanhu. (Picha na Yang Qian/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Kwenye Kituo cha kufanya mawasiliano na kujihisi cha eneo la kitaifa la majaribio ya jumla la Data kubwa la Guizhou, ambalo lipo karibu na bustani ya Guanshanhu, waandishi wa habari kutoka nchi za Eurasia walijionea matunda kemkem ya China katika maendeleo ya kizazi kipya cha TEHAMA katika mtandao wa intaneti, Data kubwa na akili bandia, na kufahamishwa zaidi historia ya maendeleo ya sekta ya Data kubwa katika mkoa wa Guizhou wa China.

Guizhou ni eneo la kwanza la kitaifa la majaribio ya jumla ya Data kubwa nchini China, na ulichukua nafasi ya kwanza kwa miaka 7 mfululizo katika ongezeko la kasi la uchumi wa kidijitali kuanzia mwaka 2015 hadi 2021 nchini China. Hivi sasa mkoa huo unafanya juhudi kubwa kuchukua fursa ya utekelezaji mapema wa mkakati wa uchumi wa kidijitali, kuharakisha kuhimiza ujenzi wa eneo la kitaifa la majaribio ya jumla ya Data kubwa la Guizhou na eneo la maendeleo na uvumbuzi la uchumi wa kidijitali, kusukuma mbele maendeleo ya mafungamano ya uchumi wa kidijitali na uchumi wa viwanda , na kuharakisha kujenga mfumo wa viwanda vya kisasa unaoongozwa na uchumi wa kidijitali.

Waandishi wa habari wakitembelea Kwenye Kituo cha kufanya  mawasiliano na kujihisi cha eneo la majaribio ya jumla  la Data kubwa la kitaifa la Guizhou. (Picha na Ynagqian/Tovuti ya Gazeti la Umma)

Waandishi wa habari wakitembelea Kwenye Kituo cha kufanya mawasiliano na kujihisi cha eneo la majaribio ya jumla la Data kubwa la kitaifa la Guizhou. (Picha na Yang Qian/Tovuti ya Gazeti la Umma)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha