Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 31, 2023
Habari ya picha ya wanandoa wapanda msitu katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Delg akifanya doria katika msitu wa Haloxylon ulioko wilaya ya Ejina ya mji wa Alxa katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, Oktoba 27, 2023. (Xinhua/Liu Jinhai)

Su He, aliyepewa jina la "mfano wa kuigwa wa nyakati hizi," ni mtumishi mstaafu anayeishi karibu na eneo la mabaki ya kale la Heicheng, mji ambao ni mkongwe uliohifadhiwa vizuri kwenye Njia ya Hariri, huko wilaya ya Ejina, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China. Su na mkewe Delg wamepanda msitu wa Haloxylon unaochukua eneo lenye ukubwa wa ekari 3,500 (kama hekta 233.33) kuanzia Mwaka 2004 hadi 2021, ambao bado unatumika kama ngao ya kiikolojia dhidi ya dhoruba za mchanga kwenye eneo hilo la mabaki ya kale la Heicheng. Delg na mtoto wao wa kiume wamebaki na kuendelea kutunza na kupanua msitu huo wa Haloxylon baada ya Su kufariki dunia Mwaka 2021.

Nyumba za bungalows zilizojengwa na Su na Delg wakati walipoanza kujikita katika jangwa Mwaka 2004 bado ziko pale, lakini sasa zimezungukwa na miti. Familia ya Su imechagua kuendelea kuishi hapa na hifadhi mazingira ya kijani katika eneo hili la jangwa ambalo hutembelewa na watu wachache.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha