Mila na Desturi mbalimbali za mwaka mpya wa jadi wa China zaonekana kwenye mitaa mikongwe ya Quanzhou (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 25, 2024
Mila na Desturi mbalimbali za mwaka mpya wa jadi wa China zaonekana kwenye mitaa mikongwe ya Quanzhou
Watu wakipita mlango wa Hekalu la Thean Hou. Kila ifikapo mwaka mpya wa jadi wa China, hekalu hilo hufungasha michele kwenye mifuko myekundu na kuiunda kwenye umbo la kobe, likiwa na makumi kwa maelfu ya kilo za uzito. Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya, watu huja kwenye hekalu hilo na kumgusa kwa kumpapasa “kobe” wa michele kutoka mwanzo hadi mwisho na kuomba baraka na kheri.

Mji mkongwe wa Quanzhou ulioko Mkoa wa Fujian, China unamiliki mabaki mengi ya kitamaduni na majengo mengi ya kale yenye thamani kubwa yanayohifadhiwa na kulindwa. Wakazi huko pia wana mila na desturi nyingi za mwaka mpya wa jadi wa China. (Picha na Huang Dongyi/People’s Daily Online)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha