Picha: hali ya kupatana kati ya binadamu na mazingira ya asili katika mji wa pwani wa Xiamen, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 21, 2024
Picha: hali ya kupatana kati ya binadamu na mazingira ya asili katika mji wa pwani wa Xiamen, China
Picha iliyopigwa Januari 24, 2024 ikionyesha Ziwa Yundang na mazingira yake yanayolizunguka huko Xiamen, Mkoa wa Fujian, Kusini Mashariki mwa China. (Xinhua/Jiang Kehong)

XIAMEN - Tangu miaka ya 1980, Mji wa Pwani wa Xiamen wa Mkoa wa Fujian, Kusini-Mashariki mwa China, haujaacha juhudi zozote za kurejesha hali ya ikolojia katika mji huo. Hadi kufikia sasa, serikali ya Mji wa Xiamen imeanzisha kampeni tano zinazolenga kurejesha hali ya ikolojia ya Ziwa Yundang. Sasa likiwa na bustani sita tofauti, kihalisi, eneo la ziwa hilo limekuwa "kituo cha burudani" kwa wakaazi.

Uzoefu uliopatikana katika mchakato huo baadaye ulianza kutumika katika juhudi kama hizo katika maeneo mengine ya mji huo. Mazingira yaliyoboreshwa yametoa fursa mpya za maendeleo ya uchumi ya mji huo, na kutoa maliasili bora kwa watu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha