Eneo la Jiuzhaigou Kusini Magharibi mwa China larejesha ustawi wake baada ya miaka ya ukarabati baada ya tetemeko (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 23, 2024
Eneo la Jiuzhaigou Kusini Magharibi mwa China larejesha ustawi wake baada ya miaka ya ukarabati baada ya tetemeko
Picha hii ya kumbukumbu iliyopigwa Mwaka 2018 ikimwonyesha Pei Xiangjun (wa kwanza kushoto) na timu yake wakifanya uchunguzi kwenye eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi katika eneo lenye mandhari nzuri la Jiuzhaigou, Mkoa wa Sichuan, Kusini-Magharibi mwa China. (Xinhua)

Bustani ya Kitaifa ya Jiuzhaigou ya China, ambayo ni eneo la Urithi wa Dunia wa UNESCO, maarufu kwa maporomoko yake ya maji ya kuvutia, misitu mirefu na maziwa ya nyanda za juu, ilikumbwa na tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 7.0 kwa kipimo cha richta Agosti 8, 2017. Baada ya tetemeko hilo, timu iliyoongozwa na profesa Pei Xiangjun kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Chengdu ilifanya kazi ya ulinzi na kukarabati mazingira ya eneo hilo la urithi wa mazingira ya asili. Baada ya miaka mingi ya ukarabati baada ya tetemeko, eneo hilo la Jiuzhaigou limepata ustawi wake tena. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha