Mavuno Mazuri ya mpunga huko Hongya, Mkoa wa Sichuan, China (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Agosti 27, 2024
Mavuno Mazuri ya mpunga huko Hongya, Mkoa wa Sichuan, China
Wanakijiji wakipakia mpunga waliovuna kwenye lori katika eneo kuu la kielelezo la "Ghala la nafaka la Tianfu" lenye ukubwa wa takriban hekta 666.67 la Anning katika mji mdogo wa Zhige, Wilaya ya Hongya, Mkoa wa Sichuan, Agosti 26(picha iliyopigwa kwa droni). (Xinhua/Xu Bingjie)

Siku hizi, eneo la kielelezo la Ghala la nafaka la Tianfu" lenye ukubwa wa takriban hekta 666.67 la Anning lililoko katika mji mdogo wa Zhige, Wilaya ya Hongya, Mji wa Meishan, Sichuan, limepata mavuno mazuri ya mpunga, na wanakijiji wamevuna mpunga katika wakati huo.

Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya ya Hongya imehimiza ujenzi wa mashamba ya kiwango cha juu, na kugeuza mashamba madogo ya awali yaliyotawanyika kuwa mashamba makubwa yanayopakana. Mwaka 2024, eneo la upandaji mpunga katika wilaya hiyo limekuwa takriban hekta 9,600.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha