Maji safi ya Bwawa la Maji la Jinpen kwenye Mto Heihe wa China yastawisha maisha ya watu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 23, 2024
Maji safi ya Bwawa la Maji la Jinpen kwenye Mto Heihe wa China yastawisha maisha ya watu
Bwawa la Maji la Jinpen la Mto Heihe lililopo Wilaya ya Zhouzhi. (Picha/Tian Gang)

Shughuli ya Kukusanya Maudhui ya Vyombo vya Habari vya Mtandaoni ya “China Nzuri 2024: Kutazama Shaanxi” imezinduliwa kwenye Kituo Kikuu cha Ulinzi wa Mlima Qinling katika Wilaya ya Eyi ya Mji wa Xi’an, Mkoa wa Shaanxi, China. Ujumbe wa waandishi wa habari wa shughuli hiyo utakwenda sehemu ya Kaskazini, Katikati na Kusini ya Mkoa wa Shaanxi, na kuingia kwa kina katika maeneo muhimu kama vile Mlima Qinling, Bonde la Mto Danjiang na Jangwa la Maowusu ili kufanya mahojiano na kuandika habari.

Baada ya hafla hiyo ya uzinduzi, ujumbe wa waandishi wa habari ulitembelea Bwawa la Maji la Jinpen kwenye Mto Heihe iliyopo Wilaya ya Zhouzhi, ambayo ni moja kati ya vyanzo vikuu vya maji katika kiini cha Mji wa Xi’an.

Bwawa hilo la maji ni mradi mkubwa wa daraja la Pili wa maji ambao hasa husambaza maji mjini, na pia una matumizi mbalimbali kama vile umwagiliaji wa kilimo, uzalishaji wa umeme na kinga dhidi ya mafuriko ya maji.

Kwa sasa baadhi ya watu waliokuwa wakiishi karibu na bwawa hilo la maji wamehamishwa kwenda kuishi sehemu zingine, hali ambayo imepunguza hatari ya uchafuzi wa maji kwenye chanzo. Wakati huohuo kundi la kampuni za mambo ya maji la Xi’an limeweka vituo vya ukaguzi katika sehemu husika, likizuia vilivyo kemikali hatari na magari yasiyohusika na mradi huo kuingia, ili kuhakikisha usalama kabisa wa chanzo hicho cha maji.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Renato Lu)

Picha