Lugha Nyingine
Mkoa wa Xinjiang wa China kuhimiza ukuaji wa viwanda vya makaa ya mawe na kusaidia maendeleo ya sifa bora ya uchumi (4)
Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China umetumia vya kutosha rasilimali zake za makaa ya mawe ili kuendeleza kwa nguvu kubwa viwanda vya makaa ya mawe na kusaidia maendeleo ya sifa bora ya uchumi.
Katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2024, uzalishaji wa mkoani Xinjiang wa makaa ghafi ya mawe kutoka kwa kampuni zenye ukubwa zaidi ya uliopangwa ulifikia tani milioni 240, ongezeko la asilimia 13.4 kuliko mwaka uliopita.
Kwa kutegemea maliasili zake nyingi za makaa ya mawe, mkoa wa Xinjiang unaharakisha uanzishaji wa mnyororo wa viwanda wa makaa ya mawe hadi mafuta na gesi, makaa ya mawe hadi olefin, na nyenzo mpya za makaa ya mawe, huku ikiwa na maendeleo ya haraka ya makundi ya viwanda ikijumuisha viwanda vya makaa ya mawe na uzalishaji umeme kwa nishati ya makaa ya mawe, pamoja na viwanda vya kemikali za makaa ya mawe.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma