Mkoa wa Xinjiang wa China kuhimiza ukuaji wa viwanda vya makaa ya mawe na kusaidia maendeleo ya sifa bora ya uchumi (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Septemba 30, 2024
Mkoa wa Xinjiang wa China kuhimiza ukuaji wa viwanda vya makaa ya mawe na kusaidia maendeleo ya sifa bora ya uchumi
Picha iliyopigwa Septemba 26, 2024 ikionyesha mwonekano wa mgodi wazi wa makaa ya mawe wa Zhundong wa Kampuni ya Nishati ya Zhundong ya Xinjiang ya Kundi la Nishati la China katika Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China. (Xinhua/Ding Lei)

Mkoa unaojiendesha wa Kabila la Wauygur wa Xinjiang, kaskazini-magharibi mwa China umetumia vya kutosha rasilimali zake za makaa ya mawe ili kuendeleza kwa nguvu kubwa viwanda vya makaa ya mawe na kusaidia maendeleo ya sifa bora ya uchumi.

Katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2024, uzalishaji wa mkoani Xinjiang wa makaa ghafi ya mawe kutoka kwa kampuni zenye ukubwa zaidi ya uliopangwa ulifikia tani milioni 240, ongezeko la asilimia 13.4 kuliko mwaka uliopita.

Kwa kutegemea maliasili zake nyingi za makaa ya mawe, mkoa wa Xinjiang unaharakisha uanzishaji wa mnyororo wa viwanda wa makaa ya mawe hadi mafuta na gesi, makaa ya mawe hadi olefin, na nyenzo mpya za makaa ya mawe, huku ikiwa na maendeleo ya haraka ya makundi ya viwanda ikijumuisha viwanda vya makaa ya mawe na uzalishaji umeme kwa nishati ya makaa ya mawe, pamoja na viwanda vya kemikali za makaa ya mawe. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha