Rais Xi awasili Kazan, Russia kwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa BRICS

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Oktoba 23, 2024
Rais Xi awasili Kazan, Russia kwa kuhudhuria mkutano wa viongozi wa BRICS
Rais wa China Xi Jinping alipeana mkono na ofisa wa Russia alipowasili kwenye uwanja wa ndege mjini Kazan, Russia, Oktoba 22, 2024. (Xinhua/Xie Huanchi)

KAZAN, Russia - Rais wa China Xi Jinping amewasili Kazan, Russia jana Jumanne kwa kuhudhuria Mkutano wa 16 wa Wakuu wa nchi za BRICS, ambapo maofisa wa Russia walimlaki Rais Xi kwenye uwanja wa ndege huku askari wa gwaride la heshima wakiwa wamejipanga pande zote za zulia jekundu kumpa heshima kiongozi huyo wa China, na vijana wa Russia waliokuwa wamevalia mavazi ya makabila wakimkaribisha kwa desturi na mila. Aidha, ndege ya kivita ya Russia ilionekana ikisindikiza ndege iliyokuwa imembeba Rais Xi. 

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Deng Jie)

Picha