Njia mpya ya usafiri wa moja kwa moja wa meli za mizigo kati ya China na kusini mashariki mwa Afrika yafunguliwa Qingdao, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Desemba 17, 2024
Njia mpya ya usafiri wa moja kwa moja wa meli za mizigo kati ya China na kusini mashariki mwa Afrika yafunguliwa Qingdao, China
Meli ya mizigo "GREEN NAGOYA" ikionekana katika Bandari ya Qingdao ya Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Desemba 16, 2024. Meli hiyo inatazamiwa kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania baada ya siku takriban 20. (Xinhua/Li Ziheng)

Njia mpya ya usafiri wa moja kwa moja wa meli za mizigo kati ya Mji wa Qingdao wa China na kusini mashariki mwa Afrika imefunguliwa rasmi jana Jumatatu. Ikiwa inatoa huduma kila wiki, njia hiyo inaongeza njia mbadala ya usafiri wa baharini iliyo salama na ya haraka kati ya China na Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha