Upendo na Ulinzi: Picha za Kumbukumbu za uokoaji wa maafa ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha 6.8 katika Wilaya ya Dingri mkoani Xizang

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Januari 09, 2025
Upendo na Ulinzi: Picha za Kumbukumbu za uokoaji wa maafa ya tetemeko la ardhi la ukubwa wa kipimo cha 6.8 katika Wilaya ya Dingri mkoani Xizang
Tarehe 8, Januari, mkazi wa Kijiji cha Tonglai cha Wilaya ya Dingri aliyeathirika katika maafa ya tetemeko la ardhi anayepakata mtoto wake akichukua nguo za kukinga baridi zilizopelekwa huko na watu wa kujitolea. (Xinhua/Jiang Fan)

Asubuhi ya tarehe 7, Januari, tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8 lilitokea katika Wilaya ya Dingri ya Mji wa Xigaze wa Xizang, China. Tetemeko hilo limesababisha vifo wa watu wengi na kubomoka kwa nyumba nyingi .

Baada ya tetemeko la ardhi kutokea, watu wa sekta mbalimbali wametoa kwa haraka msaada wao wenye moyo wa upendo na ulinzi. Timu za uokoaji zimekusanyika kwenye eneo lililoathirika katika tetemeko la ardhi, zikitafuta watu walionusurika na kulinda mali za watu kwa kadri wawezavyo.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha