China yashuhudia ongezeko la safari za watalii wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2025
China yashuhudia ongezeko la safari za watalii wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi
Watalii wakitazama ngoma ya kijadi ya simba katika Wilaya ya Tancheng ya Mji wa Linyi, Mkoa wa Shandong, mashariki mwa China, Januari 29, 2025. (Picha na Zhang Chunlei/Xinhua)

China imeshuhudia rekodi ya safari milioni 501 za watalii wa ndani wakati wa likizo ya siku nane ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi iliyomalizika Jumanne wiki hii, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.9 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya nchi hiyo jana Jumatano.

Watalii hao walitumia yuan zaidi ya bilioni 677 (dola za Kimarekani kama bilioni 94.43) katika safari zao hizo za utalii wa ndani wakati wa likizo hiyo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 kuliko mwaka jana, takwimu hizo zimeonyesha.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha