

Lugha Nyingine
China yashuhudia ongezeko la safari za watalii wakati wa likizo ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi (5)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Februari 06, 2025
![]() |
Watalii wakitembelea Eneo la Utalii wa Kitamaduni la Nanshan mjini Sanya, Mkoa wa Hainan, kusini mwa China, Januari 29, 2025. (Picha na Chen Wenwu/Xinhua) |
China imeshuhudia rekodi ya safari milioni 501 za watalii wa ndani wakati wa likizo ya siku nane ya Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi iliyomalizika Jumanne wiki hii, ikiwa ni ongezeko la asilimia 5.9 kuliko kipindi kama hicho mwaka jana, kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Wizara ya Utamaduni na Utalii ya nchi hiyo jana Jumatano.
Watalii hao walitumia yuan zaidi ya bilioni 677 (dola za Kimarekani kama bilioni 94.43) katika safari zao hizo za utalii wa ndani wakati wa likizo hiyo, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 kuliko mwaka jana, takwimu hizo zimeonyesha.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma