Tasnia ya Maua katika Mkoa wa Yunnan, China yaleta ustawi wa maisha kwa watu (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2025
Tasnia ya Maua katika Mkoa wa Yunnan, China yaleta ustawi wa maisha kwa watu
Mfanyakazi akifungasha maua freshi yaliyoagizwa kutoka Yunnan kwenye soko la maua la Pak Khlong Talat mjini Bangkok, Thailand Februari 14, 2019. Asia Kusini Mashariki ni soko la jadi la maua hayo ya Yunnan. Chini ya uhimizaji wa pendekezo la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”, ushirikiano wa kunufaishana wa kitasnia kati ya China na nchi za Asia Kusini Mashariki umeingiza uhai mpya kwenye biashara kati ya pande hizo. Kwa kufunguliwa kwa Barabara ya Kimataifa ya Kunming–Bangkok, maua freshi ya Yunnan yanaweza kufika Bangkong katika muda wa karibu saa 40 za uchukuzi wa mnyororo baridi. (Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China Juzi Jumatano mchana, Machi 19, aliwasili Eneo Maalum la Viwanda vya Kisasa vya Maua la Lijiang katika Mkoa wa Yunnan, na alikuwa na mazungumzo ya kirafiki ya ana kwa ana na wanakijiji na mafundi, akiwauliza kuhusu aina za maua, hali ya mauzo sokoni, mapato yao na mambo mengine.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa huo wa Yunnan wa China umekuwa ukifanya kazi kwa bidii kujenga “Bustani ya Dunia”, na maua, yanayoashiria maisha bora, yamekuwa kitambulisho cha kibiashara cha Yunnan.

Kuanzia “uuzaji wa barabarani” mwishoni mwa karne iliyopita, hadi hii leo kuwa na mnyororo mzima na tasnia kubwa, uchumi wa maua wa Yunnan umestawi kwa kasi na umekuwa nguvu muhimu wa kusukuma ustawishaji jumuishi na maendeleo bora ya hali ya juu ya maeneo ya vijijini.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya kila maua kumi ya kukatwa yanayouzwa kwenye soko la China, saba hutokea Kunming.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha