Tasnia ya Maua katika Mkoa wa Yunnan, China yaleta ustawi wa maisha kwa watu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 21, 2025
Tasnia ya Maua katika Mkoa wa Yunnan, China yaleta ustawi wa maisha kwa watu
Wakulima wa maua wakichukua maua freshi yaliyopangiliwa kutoka mnyororo wa kiotomatiki wa upangiliaji maua ya kukatwa, na kuyaandaa kuyapeleka kwenye mnyororo wa kufungasha katika kituo cha uchakataji maua baada ya kuyachuma cha Eneo Maalum la Viwanda vya Kisasa vya Maua mjini Jinning, Mkoa wa Yunnan, China, Agosti 23, 2024. (Xinhua)

Rais Xi Jinping wa China Juzi Jumatano mchana, Machi 19, aliwasili Eneo Maalum la Viwanda vya Kisasa vya Maua la Lijiang katika Mkoa wa Yunnan, na alikuwa na mazungumzo ya kirafiki ya ana kwa ana na wanakijiji na mafundi, akiwauliza kuhusu aina za maua, hali ya mauzo sokoni, mapato yao na mambo mengine.

Katika miaka ya hivi karibuni, Mkoa huo wa Yunnan wa China umekuwa ukifanya kazi kwa bidii kujenga “Bustani ya Dunia”, na maua, yanayoashiria maisha bora, yamekuwa kitambulisho cha kibiashara cha Yunnan.

Kuanzia “uuzaji wa barabarani” mwishoni mwa karne iliyopita, hadi hii leo kuwa na mnyororo mzima na tasnia kubwa, uchumi wa maua wa Yunnan umestawi kwa kasi na umekuwa nguvu muhimu wa kusukuma ustawishaji jumuishi na maendeleo bora ya hali ya juu ya maeneo ya vijijini.

Takwimu zinaonesha kuwa kati ya kila maua kumi ya kukatwa yanayouzwa kwenye soko la China, saba hutokea Kunming.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha