Utalii wa majira ya mchipuko waonyesha uhai wa uchumi nchini China (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Machi 26, 2025
Utalii wa majira ya mchipuko waonyesha uhai wa uchumi nchini China
Meli ikisafiri kupitia sehemu ya Mto Yangtze kwenye Genge la Xiling, katika Wilaya ya Zigui ya Mji wa Yichang, Mkoa wa Hubei, katikati mwa China, Machi 19, 2025. (Picha na Zheng Jiayu/Xinhua)

BEIJING - Wakiwa na shauku ya kuwa huru kutoka kwenye vizuizi vya majira ya baridi, watu wa China wanakumbatia shughuli mbalimbali za majira ya mchipuko huku majira hayo yakitoa fursa zisizo na kikomo za kufurahia uzuri wa mazingira ya asili.

Kadiri halijoto inavyozidi kuongezeka, shughuli zikiwemo za kutazama mandhari, kufurahia maua, kuchuma majani ya chai, na kwenda sokoni zimechochea "uchumi wa majira ya mchipuko" unaostawi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha