Robert Francis Prevost achagualiwa kuwa Papa Leo XIV (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 09, 2025
Robert Francis Prevost achagualiwa kuwa Papa Leo XIV
Robert Francis Prevost (wa pili kulia) akipungia mkono umati baada ya kuchaguliwa kuwa papa mpya katika mji wa Vatican, Mei 8, 2025. (Xinhua/Li Jing)

ROMA - Robert Francis Prevost, Kardinali wa Kanisa Katoliki la Marekani, amechaguliwa kuwa papa mpya wa Kanisa hilo katika siku ya pili ya kura za siri kwenye kongamano la Makadinali lililofanyika mjini Vatican ambapo jina alilochagua kuwa papa mpya ni Leo XIV.

Chuo cha Makardinali, chenye makadinali 133, kilianza mchakato wa upigaji kura kwa siri kumchagua papa mpya Mei 7. Papa wa awali, Francis, aliaga dunia kutokana na ugonjwa Aprili 21.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha