

Lugha Nyingine
Mashindano ya lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yafanyika nchini Kenya
![]() |
Mshiriki akishiriki katika Mashindano ya 24 ya Daraja la Lugha ya Kichina kwa Wanafunzi wa Vyuo yaliyofanyika kwenye Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, Mei 7, 2025. (Xinhua/Li Yahui) |
NAIROBI - Mashindano ya 24 ya Umahiri wa Lugha ya Kichina ya Daraja la Lugha ya Kichina kwa Wanafunzi wa Vyuo vikuu nchini Kenya yamefanyika katika chuo kikuu kikongwe zaidi nchini humo, Chuo Kikuu cha Nairobi, chini ya kaulimbiu ya "Dunia Moja, Familia Moja" ambapo maofisa waandamizi, wanadiplomasia, wadau wa tasnia, wanafunzi na wasomi walishiriki kwenye shughuli hiyo ya nusu siku ambayo ilijumuisha hotuba na maonyesho ya kitamaduni, ikiwemo opera ya Beijing.
Washindi kumi na tisa waliotoka katika Taasisi nne za Confucius zinazoendeshwa na vyuo vikuu vya umma nchini Kenya walishiriki katika mashindano hayo yaliyojumuisha sehemu mbili -- kutoa hotuba katika lugha sanifu ya Kichina na maonyesho ya vipaji.
Wakati wa sehemu ya hotuba, washindani walitoa simulizi za safari zao kwa lugha ya Kichina na kuelezea matarajio yao ya maelewano ya tamaduni tofauti na mapatano ya dunia kupitia hotuba yao.
Katika sehemu ya maonyesho ya vipaji, washiriki walionyesha upendo wao kwa utamaduni wa China kupitia maonyesho mbalimbali -- wengine walicheza dansi wakivaa Hanfu (vazi la jadi la Kichina), wengine waliandikia maandishi ya Kichina kwa umaridadi, huku wengine wakivalia vinyago vya Opera ya Beijing ili kukariri au kuimba.
Ukumbi ulikuwa umejaa kwa wingi, huku watazamaji wengi wakisimama wakati wote wa tukio hilo, na nderemo na vifijo vikisikika mara kwa mara.
Miongoni mwa washiriki ni Catherine Wangari mwenye umri wa miaka 25 kutoka Chuo Kikuu cha Moi, ambaye alitumia jina la Kichina la Wang Menglin. Alivutia hadhira kwa kuimba wimbo wa Kichina "Marafiki," akishangiliwa sana.
"Ninasoma Kichina kwa bidii sasa, nikitumai kufanya kazi katika hoteli baada ya kuhitimu na kukaribisha watalii wa China kwa ufasaha," amesema Wangari, mwanafunzi wa usimamizi wa ukarimu anayetarajiwa kuhitimu mwaka huu.
"Katika miaka ya hivi karibuni, kuongezeka kwa wageni wa China nchini Kenya kumetoa nafasi nyingi za ajira na kuongeza mapato kwa sekta ya utalii." Amoengeza.
Baada ya saa nne za ushindani mkali na mashauri makali ya majaji, Naomi Wanjiku Thuo kutoka Taasisi ya Confucius katika Chuo Kikuu cha Nairobi alitwaa ubingwa wa Fainali za Raundi ya Kenya ya "Daraja la Lugha ya Kichina" mwaka huu.
Kwa umahiri wake bora wa Kichina, tafsiri ya kina ya kaulimbiu, na maonyesho mazuri y kipaji, Thuo ataiwakilisha Kenya kwenye fainali za kimataifa nchini China.
Wanafunzi wengine watano walitunukiwa zawadi za pili na tatu, huku tuzo nyingine zikiwemo Tuzo ya Kipaji Bora, Tuzo ya Charisma Bora, Tuzo ya Ufasaha Bora, na Tuzo ya Nyota Anayeibukia pia zilitolewa.
Kabla ya mashindano hayo kulifanyika hafla ya Tuzo ya "Ufadhili wa Masomo wa Balozi wa China" ambapo balozi wa China nchini Kenya Guo Haiyan alitoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 30 kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
Margaret Hutchinson, naibu mkuu wa Chuo Kikuu cha Nairobi, amesema Ufadhili wa Masomo wa Balozi wa China" umewezesha wanafunzi wengi kukamilisha masomo yao na kufikia matarajio yao ya taaluma.
Amesema mashindano ya "Daraja la Lugha ya Kichina" yameongeza shauku ya kujifunza lugha ya Kichina, viwango vya juu vya umahiri, na uelewa wa kina wa ushirikiano kati ya China na Kenya na jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja kupitia kaulimbiu ya "Dunia Moja, Familia Moja."
Kwa upande wake Guo amesema mpango wa ufadhili wa masomo ni hatua madhubuti ya kufikia maono ya pamoja ya China na Kenya.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma