China yarusha satalaiti mpya za kuhisi kwa mbali kwenda anga ya juu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2025
China yarusha satalaiti mpya za kuhisi kwa mbali kwenda anga ya juu
Roketi ya Long March-6 iliyorekebishwa ambayo ilibeba seti ya satalaiti za Yaogan-40 02 ikirushwa kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Taiyuan, Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China, Mei 11, 2025. (Picha na Zheng Taotao/Xinhua)

TAIYUAN – China imerusha seti ya satalaiti za kuhisi kwa mbali kwenda anga ya juu kutoka Kituo cha Kurushia Satalaiti cha Taiyuan katika Mkoa wa Shanxi, kaskazini mwa China siku ya Jumapili.

Zikiwa zimerushwa majira ya saa 3:27 usiku (kwa saa za Beijing) ndani ya roketi ya Long March-6 illiyorekebishwa, satalaiti hizo za Yaogan-40 02 zimeingia  kwa mafanikio kwenye obiti iliyopangwa, kampuni mrushaji imeeleza.

Kampuni hiyo imeeleza kuwa, satalaiti hizo zitatumika kufanya ukaguzi na ufuatiliaji wa mazingira ya sumaku-umeme na majaribio ya teknolojia husika.

Urushaji huo wa jana Jumapili ni safari ya 574 kufanywa na mfululizo wa roketi ya Long March, kituo hicho kimeeleza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha