Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China (4)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2025
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
Wakulima wakiendesha trekta lenye mfumo wa urambazaji wa Beidou kwa ajili ya kupanda mbegu katika wilaya ya Horqin ya Mji wa Tongliao, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China, Mei 9, 2025. (Xinhua/Lian Zhen)

Ikinufaika na mvua zinazonyesha kwa wakati wa Mei, Tongliao, ghala la chakula katika mashariki mwa Mkoa wa Mongolia ya Ndani, kaskazini mwa China, imeingia katika kipindi cha kilele cha kupanda nafaka. Habari zinasema kuwa ukubwa wa eneo la kupanda mahindi la Tongliao mwaka 2025 unatarajiwa kufikia mu milioni 20 (hekta takriban milioni 1.33), ikiongeza mu 180,000 (hekta 12,000) kulinganishwa na mwaka uliopita. 

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha