

Lugha Nyingine
Gavana wa California aonya kuhusu dharura ya kiuchumi ya "tahadhari nyekundu" kutokana na ushuru wa juu
![]() |
Picha hii iliyopigwa Mei 10, 2025 ikionyesha mwonekano wa Bandari ya Los Angeles jimboni California, Marekani. (Picha na Qiu Chen/Xinhua) |
SACRAMENTO, Marekani - Katika tangazo la hivi karibuni, Gavana wa Jimbo la California, Gavin Newsom ameonya umma wa Marekani kuhusu matokeo "halisi" na "mabaya" ya ushuru wa juu wa hivi karibuni, akielezea hali hiyo kuwa ni "tahadhari nyekundu"ya dharura ya kiuchumi.
"California sasa ni ya nne kwa uchumi mkubwa duniani. Uvumbuzi, viwanda, kilimo. Na tumefikia hali hiyo kwa kupunguza vizuizi vya biashara na kutimiza ahadi kwa watumiaji wa Marekani," Newsom amesema katika tangazo hilo lililochapishwa mtandaoni Ijumaa.
"Lakini utawala wa Trump unaweka yote hayo hatarini, ukizuia uwasilishaji wa bidhaa muhimu kupitia bandari zetu. Leo, ni mabegi ya shule. Katika miezi michache baadaye, itakuwa midoli ya Krismasi," amesema.
Kwenye mahojiano yaliyorushwa Jumamosi, Newsom ameeleza kwamba alirusha tangazo hilo kwenye kituo cha televisheni cha kihafidhina cha Fox News wikendi hii (wikiendi iliyopita), akitumai utawala wa Marekani "unaelewa na kushughulikia athari hizo."
Aidha, Newsom ameonyesha hali ya hatari zaidi kwenye mahojiano yake hayo, akisema dharura ya kiuchumi ya "tahadhari nyekundu" imeanzishwa na sera hizo za ushuru, ambazo tayari zimeshaathiri vibaya bandari kubwa za California.
Gavana huyo amesema kuwa, Bandari ya Oakland kaskazini mwa California ilikuwa imekumbwa na upungufu wa asilimia 20 wa kiasi cha shehena, wakati huohuo bandari za Long Beach na Los Angeles kusini mwa California zimeripoti punguzo la asilimia 35, huku oda za mizigo zikishuka kwa asilimia 60.
Matokeo haya hayawezi kutatuliwa kwa urahisi au haraka. "Inachukua wiki kadhaa kwa maamuzi yaliyofanywa nchi za nje na oda za ununuzi kuanza kutekelezwa kabla ya bidhaa kufikia kwenye rafu. Maamuzi yanayofanywa leo -- au kutokuwa na uamuzi kuhusu dhamira - kutakuwa na athari kubwa kesho," amesema, akiongeza kuwa hata kama sera hizo zingetenguliwa mara moja, athari zitaendelea kuwepo katika miezi ijayo.
Newsom amekuwa ikisema wazi kwamba California imeathiriwa vibaya na ushuru huo wa juu. Wakati huo huo, California lilikuwa jimbo la kwanza la Marekani kuwasilisha kesi mahakamani dhidi ya serikali kuu ya Marekani juu ya masuala ya ushuru.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma