

Lugha Nyingine
Wang Yi akutana na wageni wanaoshiriki katika mkutano wa nne wa mawaziri wa Baraza la China-CELAC (8)
![]() |
Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Guyana Hugh Todd, mjini Beijing, mji mkuu wa China, Mei 12, 2025. (Xinhua/Yue Yuewei) |
BEIJING - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Jumatatu kwa nyakati tofauti alikutana na baadhi ya mawaziri wa mambo ya nje na wawakilishi wa nchi wanaohudhuria mkutano wa nne wa mawaziri wa Baraza la China na CELAC (Jumuiya ya Nchi za Latin Amerika na Caribbean) mjini Beijing.
Wakati akikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Cuba Bruno Rodriguez Parrilla, Wang amesema kuwa Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Cuba Miguel Diaz-Canel walifanya mkutano muhimu wenye matunda mjini Moscow, wakiweka dira ya upigaji hatua zaidi katika uhusiano kati ya China na Cuba.
Amesema, China itaendelea kuiunga mkono Cuba katika mapambano yake ya haki ya kulinda mamlaka na hadhi ya taifa na kupinga vizuizi na vikwazo, na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya China na Cuba yenye mustakabali wa pamoja ili kuendelea kufikia maendeleo mapya.
Kwa upande wake Rodriguez ametoa shukrani za dhati kwa China kwa kuunga mkono Cuba kithabiti katika kupinga vizuizi na vikwazo, vilevile msaada wake muhimu kwa Cuba kuondokana na matatizo ya kiuchumi.
Wakati akikutana na waziri wa mambo ya nje wa Uruguay Mario Lubetkin, Wang amesema kuwa China inapenda kushirikiana na Uruguay ili kuzidisha ushirikiano wa kiwango cha juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja na kuendelea kuimarisha uhusiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Uruguay kwa hali imara zaidi ya kuaminiana kisiasa, ushirikiano wa ngazi ya juu zaidi wa kunufaishana na ushirikiano wa karibu zaidi wa pande nyingi.
Naye Lubetkin amesema kuwa Uruguay inathamini sana mapendekezo yaliyotolewa na Rais Xi, inaunga mkono biashara huria na ingependa kushirikiana kutekeleza mfumo wa pande nyingi, akiongeza kuwa upande wa Uruguay unafuata kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja na inaunga mkono sera ya "nchi moja, mifumo miwili".
Alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Peru Elmer Schialer Salcedo, Wang amesema kuwa Rais Xi na Rais Dina Boluarte wa Peru walitembeleana mwaka jana, akibainisha kuwa China inapenda kutekeleza maafikiano muhimu yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili na kuhimiza ushirikiano wa kimkakati wa pande zote kati ya China na Peru kufikia kiwango kipya.
Kwa upande wake Schialer amesema kuwa Peru inafuata kwa dhati kanuni ya kuwepo kwa China moja, inatarajia kuzidisha ushirikiano wa pande zote na China katika siasa, uchumi, biashara, sayansi, teknolojia, utamaduni na kadhalika, na inapenda kujenga kwa pamoja Eneo Maalum la Viwanda la Bandari ya Chancay, kuhimiza zaidi ushirikiano wa biashara huria kati ya nchi hizo mbili, na kuharakisha mazungumzo na kusainiwa kwa makubaliano ya kukwepa kutozana ushuru mara mbili.
Wang pia alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil, Waziri wa Mambo ya Nje wa Guyana Hugh Todd, Mshauri wa Rais wa Nicaragua Laureano Ortega Murillo na waziri wa mambo ya nje wa Nicaragua Valdrack Ludwing Jaentschke Whitaker na waziri wa mambo ya nje wa Colombia Laura Sarabia.
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
Shaolin Kungfu, chombo muhimu cha mawasiliano ya Utamaduni wa China na ulimwengu wa nje
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma