Shughuli kuu ya China ya Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho 2025 yafanyika Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2025
Shughuli kuu ya China ya Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho 2025 yafanyika Beijing
Watembeleaji wakitazama vitu kwenye "Maonyesho Mfululizo juu ya Asili ya Ustaarabu wa China: Hii ni Enzi ya Shang" kwenye Jumba la Makumbusho ya Mfereji Mkuu la Beijing, Mei 18, 2025. (Xinhua/Chen Zhonghao)

BEIJING – Yakiwa na kaulimbiu "Mustakabali wa Majumba ya Makumbusho katika maeneo ya makazi yanayobadilika haraka", shughuli kuu ya China ya Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho 2025 imefanyika kwenye Jumba la Makumbusho ya Mfereji Mkuu la Beijing jana Jumapili.

Kwenye hafla ya kuanzishwa kwa shughuli hiyo, orodha ya Uteuzi wa Majumba ya Makumbusho ya China yenye nguvu zaidi ya ubunifu ya mwaka 2025 na tuzo ya kazi bora ya "Maonyesho Kumi Bora ya Majumba ya Makumbusho" (ya mwaka 2024) nchini China ilitolewa, na shughuli za Beijing za majumba ya makumbusho mwaka 2025 zimeanzishwa rasmi.

"Maonyesho Mfululizo juu ya Asili ya Ustaarabu wa China: Hii ni Enzi ya Shang" pia yamefunguliwa, yakionyesha vitu 338 vya mabaki ya kitamaduni yenye thamani kutoka kwa taasisi 28 za kiakiolojia na kitamaduni kote nchini China, vinavyohusisha maandishi yaliyoandikwa kwenye mifupa ya kobe, vyombo vya shaba nyeusi, vyombo vya udongo na jade, na vingine kadhaa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha