

Lugha Nyingine
Jumba la Makumbusho ya viwanda vya Zana za Mashine la Tianjin laanza kufanya kazi kwa majaribio katika Siku ya Kimataifa ya Makumbusho
![]() |
Watu wakitembelea Jumba la Makumbusho ya Viwanda Vya Zana za Mashine la Tianjin mjini Tianjin, kaskazini mwa China, Mei 18, 2025. (Xinhua/Sun Fanyue) |
Jumba la Makumbusho ya Viwanda vya Zana za Mashine la Tianjin, lililojengwa kwa kugeuzwa kutoka eneo la zamani la kiwanda cha Kampuni ya kwanza ya Zana za Mashine ya Tianjin, limeanza kufanya kazi kwa majaribio katika Siku ya Kimataifa ya Majumba ya Makumbusho, jana Jumapili, Mei 18.
Jumba hilo la makumbusho lina eneo la maonyesho la kudumu lenye ukubwa wa mita za mraba 1,100 linaloonyesha zaidi ya zana 40 za mashine na vitu vya zamani vya kiviwanda zaidi ya 200, nyaraka na picha za kumbukumbu.
Kikiwa kilianzishwa mwaka 1951, kiwanda hicho cha Kampuni ya kwanza ya Zana za Mashine ya Tianjin kiliwahi kuwa mwanzilishi wa mfano katika sekta ya zana za mashine za gia ya China. Kama sehemu ya juhudi za ukarabati na uhuishaji wa mjini za Tianjin, eneo hilo limehuishwa na kuwa alama ya kitamaduni inayochanganya elimu ya kiviwanda na utalii, likihifadhi urithi wa utengenezaji bidhaa wa mji huo.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma