

Lugha Nyingine
Wamalaysia wawaaga kwa machozi panda wawili Xing Xing na Liang Liang
![]() |
Watu wenyeji wakiwaaga panda Xing Xing na Liang Liang nje ya Bustani ya Wanyama ya Negara karibu na Kuala Lumpur, Malaysia, Mei 18, 2025. (Picha na Chong Voon Chung/Xinhua) |
KUALA LUMPUR - Wamalaysia wamewaaga kwa machozi panda wawili Xing Xing na Liang Liang jana Jumapili, ambao watarejea China baada ya kuwepo kwao kwa miaka 11 katika nchi hiyo ya Asia Kusini-Mashariki ambapo makumi ya watakia kila la kheri na mashabiki wa panda hao pendwa walikusanyika mapema majira ya saa 11 alfajiri kwenye Kituo cha Uhifadhi Panda cha Bustani ya Wanyama ya Zogara, kuwaaga, huku wengine wakisafiri kutoka majimbo mengine kwenda kwenye bustani hiyo ya wanyama ya kitaifa iliyoko katika mji mkuu, Kuala Lumpur.
Wakati magari yakiwasili kuwasafirisha Xing Xing na Liang Liang hadi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kuala Lumpur, wengi wamesisimuka sana na kuwapungia kwa huzuni mkono wa kwaheri panda hao, huku baadhi wakipiga picha na video za kuwakumbuka.
Miongoni mwa waliokusanyika ni naibu mkuu wa Bustani ya Wanyama ya Negara Rosly Rahmat Ahmat Lana, ambaye amesema mlezi wa panda Mohd Saiffullah Md Yusuf atafuatana na panda hao hadi China na kukaa kwa siku chache ili kuwasaidia kutulia.
"Panda wana afya njema. Siku zote tumekuwa tukiunga mkono mpango wa uhifadhi wa panda. Nawashukuru sana mashabiki waliofika...uwepo wao unaonyesha namna gani wanavyojali," amewaambia waandishi wa habari.
Panda hao wawili walikopeshwa kwa serikali ya Malaysia mwaka 2014 kwa miaka 10 ili kuadhimisha miaka 40 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Malaysia na China.
Wametoa mchango mkubwa wa kuwa "mabalozi" wa nchi, kuimarisha uhusiano wa pande mbili kupitia maelfu ya watembeleaji wa Malaysia waliokuja kuwaona na kujifunza kuhusu jitihada za uhifadhi zinazofanywa na China kupitia taarifa zilizopatikana katika kituo walichokuwa wamewekwa.
Panda hao wawili wamebarikiwa kupata vitoto vitatu wakati wa kuwepo kwao Malaysia -- Nuan Nuan, aliyezaliwa mwaka 2015, Yi Yi, aliyezaliwa mwaka 2018, na Sheng Yi, aliyezaliwa mwaka 2021. Wote watatu walirudishwa China salama kabla ya wazazi wao hao kurudi.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma