Mashindano ya umahiri wa lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yafanyika nchini Misri (5)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 19, 2025
Mashindano ya umahiri wa lugha ya Kichina kwa wanafunzi wa vyuo vikuu yafanyika nchini Misri
Ola Sherief (wa pili kulia), mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Cairo, akishangilia na marafiki baada ya kushinda tuzo kuu kwenye mashindano ya kimataifa ya 24 ya umahiri wa Lugha ya Kichina ya "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri mjini Cairo, Misri, Mei 17, 2025. (Xinhua/Wang Dongzhen)

CAIRO - Mashindano ya kimataifa ya 24 ya umahiri wa Lugha ya Kichina ya "Daraja la Lugha ya Kichina" kwa wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri yamekamilika juzi Jumamosi katika mji mkuu wa Misri, Cairo ambapo mashindano hayo, yaliyoandaliwa na Ubalozi wa China nchini Misri na kuratibiwa na Klabu ya Daraja la Lugha ya China yenye makao yake mjini Cairo, lilikuwa na sehemu tatu: hotuba, chemsha bongo ya maarifa, na maonyesho ya vipaji.

Washindi kumi na wawili walifuzu kutoka kwenye washiriki 30 waliokuwa wakiwakilisha vyuo vikuu 24 vya Misri katika raundi za awali. Washiriki walionyesha kiwango cha juu cha lugha ya Kichina na uelewa wa kina wa mambo ya China.

Wanafunzi wawili kutoka Chuo Kikuu cha Cairo, Ola Sherief na Youssef Ehab, walishinda tuzo kuu na tuzo ya kwanza mtawalia.

Mshindi wa tuzo kuu Sherief, mwanafunzi anayesomea utafsiri wa lugha ya Kichina amesema anapenda kujifunza lugha ya Kichina na kuelewa utamaduni wa Kichina kupitia filamu na televisheni za Kichina na majukwaa ya mitandao ya kijamii wakati wa baada ya masomo.

"Natumai kutumia lugha ya Kichina kama daraja la kutoa mchango kwa ajili ya maelewano na mawasiliano ya kitamaduni kati ya vijana wa China na Misri," Sherief ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua.

“Tunakaribisha vijana zaidi wa Misri kutembelea China na kutoa mchango wao katika kuhimiza mmawasiliano ya kitamaduni kati ya China na Misri, kuhimiza kufunzana na kunufaishana miongoni mwa ustaarabu mbalimbali wa dunia, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu.” Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Elimu na Ushirikiano wa Lugha cha China, Liu Jianqing, amesema.

Misri imefungua kozi 32 za Lugha ya Kichina katika vyuo vikuu 30, na shule za sekondari za umma 21 zimeanzisha lugha ya Kichina kama somo la kuchaguliwa kwa lugha ya pili ya kigeni.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha