Trump asema mazungumzo ya simu na Putin "yamekwenda vizuri sana"

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2025
Trump asema mazungumzo ya simu na Putin
Rais Donald Trump wa Marekani na mkewe Melania Trump wakiwasili kwa hafla ya kusainiwa kwa Sheria ya Kuondoa Mtandaoni katika Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Mei 19, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

LOS ANGELES - Rais Donald Trump wa Marekani katika ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii baada ya mazungumzo ya saa mbili ya simu kuhusu vita vya Ukraine na mwenzake wa Russia Vladimir Putin amesema mazungumzo hayo "yamekwenda vizuri sana", akisema Russia na Ukraine zitaanzisha mazungumzo ya upatanishi ambayo masharti yanaweza tu kuwekwa na pande hizo mbili zenyewe.

"Russia na Ukraine mara moja zitaanza mazungumzo ya upatanishi kuhusu Kusimamisha mapigano na, muhimu zaidi, MWISHO wa Vita," Trump ameandika, akiongeza kuwa "masharti ya hilo yatajadiliwa kati ya pande hizo mbili, kwani inawezekana tu, kwa sababu wanajua mambo halisi ya mazungumzo ya upatanishi ambayo hakuna mwingine anaweza kujua."

Trump amesema kuwa Russia inataka "kufanya BIASHARA kubwa na Marekani" wakati hali mbaya ya sasa ikiwa imekwisha na akaelezea imani yake kuwa Ukraine inaweza kunufaika kutoka kwenye biashara vilevile.

"Kuna fursa kubwa kwa Russia kutengeneza idadi kubwa ya ajira na utajiri. Uwezekano wake kifursa ni USIO NA KIKOMO. Vile vile, Ukraine inaweza kuwa mnufaika mkubwa wa Biashara, katika mchakato wa kujenga upya Nchi yake," ujumbe huo unasomeka.

Trump pia amesema ameambia Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky na viongozi wengine kuhusu mawasiliano hayo ya simu, akiwemo Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni, Chansela wa Ujerumani Friedrich Merz na Rais wa Finland Alexander Stubb.

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha