

Lugha Nyingine
Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani wafunguliwa mjini Geneva kwa kufuatilia "Dunia Moja kwa Afya"
![]() |
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akizungumza kwenye Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani mjini Geneva, Uswisi, Mei 19, 2025. (Xinhua/Lian Yi) |
GENEVA - Mkutano wa 78 wa Baraza la Afya Duniani (WHA) umefunguliwa jana Jumatatu mjini Geneva, Uswizi, chini ya kaulimbiu ya "Dunia Moja kwa Afya" ambapo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus akihutubia hafla ya ufunguzi amesema kuwa kila mkutano huo ni muhimu, lakini mkutano wa mwaka huu ni wa kihistoria kwani nchi wanachama zinatarajiwa kujadili na kuwa na uwezekano wa kupitisha makubaliano ya kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa.
Tedros pia ametoa wito kwa nchi wanachama kuidhinisha raundi inayofuata ya ongezeko la ufadhili ili kusaidia kuhakikisha uendelevu wa kifedha wa muda mrefu na kujitegemea kwa WHO.
Lei Haichao, mkuu wa Kamisheni ya Kitaifa ya Afya ya China na kiongozi wa ujumbe wa China, ametoa taarifa kwenye mjadala wa Jumatatu, akisisitiza ushiriki kikamilifu wa China katika ushirikiano wa afya duniani.
Amesema katika kipindi cha miongo sita iliyopita, China imetuma zaidi ya wahudumu wa afya 30,000 katika nchi na maeneo 77, wakitoa matibabu kwa wagonjwa zaidi ya milioni 300. Na kwamba wakati wa janga la COVID-19, China ilitoa vifaa kinga bilioni 500 na dozi bilioni 2.3 za chanjo duniani.
Lei amesisitiza kuwa China itaendelea kuunga mkono WHO na ushirikiano wa pande nyingi kupitia hatua halisi. Amekaribisha mageuzi ya ndani ya shirika hilo na kueleza nia ya China kushirikiana na nchi nyingine wanachama ili kujenga jumuiya ya kimataifa ya afya kwa wote.
Pia amesema Taiwan ni sehemu isiyotengeka ya China na WHA kwa muda mrefu imekuwa ikifanya maamuzi dhahiri ya kutojumuisha katika ajenda yake kile kinachoitwa pendekezo la ushiriki wa Taiwan katika mkutano huo wa mwaka kama mwangalizi.
“Kauli zilizotolewa na baadhi ya nchi kuhusu Taiwan zimevuruga ajenda na kwenda kinyume na nia ya jumuiya ya kimataifa,” amesema, akiongeza kuwa China inazitaka nchi hizo kuacha kuingilia masuala yake ya ndani.
Lengo kuu la mkutano wa mwaka huu ni kujadili makubaliano ya maambukizi ya ugonjwa ambayo yamekuwa yakitarajiwa sana. WHO ilitangaza Aprili 16 kwamba, kufuatia zaidi ya miaka mitatu ya majadiliano ya kina, nchi wanachama zimefikia mwafaka juu ya mswada wa makubaliano hayo.
Wajumbe pia watapitia ripoti ya matokeo ya 2024 na kuangazia karibu vipengee 75 vya ajenda zinazohusu mada mbalimbali, zikiwemo za nguvu kazi ya afya na wahudumu, ukinzani wa antimicrobial, hali ya dharura ya kiafya, polio na mabadiliko ya tabianchi, miongoni mwa masuala mengine.
Mkutao wa mwaka huu umepangwa kukamilika Mei 27.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma