

Lugha Nyingine
Xi Jinping asisitiza kuwa na imani kithabiti kwa maendeleo ya sifa bora ziarani Henan
ZHENGZHOU - Rais Xi Jinping katika ziara yake ya ukaguzi wa miji ya Luoyang na Zhengzhou katika Mkoa wa Henan siku ya Jumatatu na jana Jumanne amesisitiza kuwa na imani kithabiti kwa kuhimiza maendeleo ya sifa bora na kuimarisha uwezo na ufanisi wa utawala, huku akiutaka mkoa huo wa katikati mwa China kuandika ukurasa mpya wa ujenzi wa mambo ya kisasa wa China.
Rais Xi, ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya China (CMC) amesisitiza kuwa, Henan inapaswa kuweka mkazo zaidi katika ujenzi wa mfumo wa viwanda vya kisasa na kuimarisha uwezo wake wa kilimo, kuongeza ustawi wa watu na kuinua kiwango cha usimamzi wa jamii, kuimarisha ulinzi wa mazingira ya kiikolojia, na kuhimiza ustawi wa kiutamaduni.
Siku ya Jumatatu alasiri, Rais Xi alitembelea Kampuni ya Kundi la Luoyang Bearing. Kampuni hiyo awali ilikuwa kiwanda kilichoanzishwa wakati wa kipindi cha utekelezaji wa mpango wa kwanza wa maendeleo ya miaka mitano wa China (1953-1957). Mpango huo wa maendeleo ya miaka mitano uliweka msingi wa kiviwanda kupitia juhudi kubwa za kujenga kituo cha kwanza cha uzalishaji chuma cha Jamhuri ya Watu wa China na kampuni ya kwanza ya uundaji wa magari.
Rais Xi alisema, katika mchakato wa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya China, ni muhimu kudumisha hali tulivu na thabiti ya viwanda vya uzalishaji bidhaa, ambavyo ni nguzo kuu ya uchumi wa nchi.
Siku hiyo Rais Xi pia alitembelea Hekalu la Farasi Mweupe lililojengwa wakati wa Enzi ya Han Mashariki (25-220), ambako alifahamishwa kuhusu dini ya Kibuddha ilivyojitahidi kufuatia mazingira ya kidini ya China, na wakazi wa huko wanavyofanya jitihada za kuhifadhi mabaki ya kale ya kitamaduni.
Alipokuwa katika Magofu ya Longmen, eneo la Mali ya Urithi ya Dunia kwenye orodha ya UNESCO lenye umri wa miaka zaidi ya 1,500 ambalo pia linawakilisha kilele cha sanaa ya uchongaji wa mawe ya China, Rais Xi alisisitiza umuhimu wa kuhifadhi, kurithi na kuendeleza hazina hizo za utamaduni wa China.
Rais Xi alisema, mafungamano ya utamaduni na utalii yana nguvu kubwa ya kuleta ustawi, ni lazima kufanya juhudi za kuhimiza maendeleo ya sifa bora ya sekta hiyo na kuifanya kuwa nguzo ya shughuli zinazoleta manufaa kwa watu na kuboresha maisha yao.
Jana Jumanne asubuhi, Rais Xi alisikiliza ripoti ya kazi ya mamlaka za mkoa huo. Amesisitiza kuwa maendeleo ya sifa bora ni msingi wa kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa wa China na kutokana na mazingira magumu ya nje, China inapaswa kukusanya nguvu zote katika kusimamia vizuri mambo ya ndani na kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.
Rais Xi ametoa wito wa kufanya juhudi halisi za kudumisha utulivu wa ajira, biashara, soko na matarajio.
Kwa vile ukame umekuwa ukinyemelea katika baadhi ya mikoa nchini China tangu mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Xi ametoa wito wa ugawaji bora wa maji, kuhakikisha usambazaji maji kwa wakazi na kukidhi mahitaji ya kilimo cha umwagiliaji.
Ameiagiza mikoa yote kufanya maandalizi ya kina kwa ajili ya kuzuia na kudhibiti mafuriko wakati msimu wa mafuriko unapowadia.
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
Maonyesho ya Kimataifa ya Baiskeli ya China 2025 yaanza Shanghai
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma