Ujenzi waahirishwa ili kulinda korongo weupe wa mashariki katika Mkoa wa Anhui, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2025
Ujenzi waahirishwa ili kulinda korongo weupe wa mashariki katika Mkoa wa Anhui, China
Picha iliyopigwa kwa droni tarehe 21 Mei, 2025 ikionyesha korongo weupe wa mashariki wakitunza vifaranga kwenye kiota kilicho juu ya mnara wa kusambaza umeme katika Wilaya ya Huoqiu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China. (Xinhua/Zhou Mu)

Mapema Mei mwaka huu, wafanyakazi waligundua kiota cha korongo mweupe wa mashariki, ndege anayeishi kwa kuhama-hama aliye chini ya ulinzi wa ngazi ya juu wa nchi ya China, kwenye mnara mpya wa kusambaza umeme katika Wilaya ya Huoqiu, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China.

Kampuni ya Gridi ya Kitaifa ya Anhui Electric Power imefunga kamera za kuonesha picha kwa ubora wa hali ya juu karibu na kiota hicho, kuwapa jukumu wafanyakazi kufuatilia na kulinda korongo hao weupe wa mashariki, na kuahirisha hatua za ujenzi kulingana na ratiba ya kutotoa na kukuza vifaranga kwa korongo hao.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha