AI yasaidia kuhimiza maendeleo ya biashara katika Mji wa Yiwu, China

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2025
AI yasaidia kuhimiza maendeleo ya biashara katika Mji wa Yiwu, China
Sun Lijuan akionekana katika picha katika Mji wa Biashara ya Kimataifa wa Yiwu Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, Mei 20, 2025. (Xinhua/Han Chuanhao)

Sun Lijuan ni miongoni mwa wafanyabiashara wa kwanza kutumia teknolojia ya AI kwa kufanya biashara na wageni katika Mji wa Biashara ya Kimataifa wa Yiwu, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China. Mji wa Yiwu ni kituo cha kimataifa cha uzalishaji na uuzaji wa bidhaa ndogo ndogo. Duka lake, Hongsheng Toys, linauza midoli inayofanania viumbe halisi na midoli pendwa ya wanyama kwa wateja wa kimataifa.

Katika miaka ya hivi karibuni, maendeleo ya haraka ya AI yamekuwa yakiongeza oda zake na kusaidia kupunguza gharama za uendeshaji. Kwa kutumia teknolojia ya AI, Sun anaweza kuwasilisha video zinazouza bidhaa katika matoleo ya lugha 36 tofauti kwa watazamaji wa kimataifa. Hata mienendo ya midomo ya wasemaji kwenye video hizo inaweza kubadilika kulingana na matamshi.

Sasa katika mji huo wa Yiwu, wafanyabiashara karibu 30,000 wanatumia zana mbalimbali za AI mara kwa mara katika biashara zao. Programu husika za AI zilizobuniwa Yiwu pekee zimekusanya watumiaji zaidi ya bilioni moja.

Mbali na kurekodi video za uuzaji bidhaa, Sun anashughulikia masuala yote yanayohusu biashara yake ndani ya duka la mita 13.5 za mraba mwaka mzima.

Kukumbatia teknolojia mpya kama vile AI kunahesabiwa kama moja ya sababu ya biashara inayostawi ya Sun. Anatumai kuwa AI itaweza kunufaisha wafanyabiashara zaidi wa Yiwu.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha