

Lugha Nyingine
Sheria mpya ya kuandikisha ndoa ya China yachochea utalii na matumizi
![]() |
Wanandoa wakifanya harusi katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Wabai la Dali, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Mei 10, 2025.(Xinhua) |
BEIJING – Juzi Jumanne asubuhi, tarehe 20, Yang Min na bibi harusi wake, He Xingyue, waliandikisha ndoa yao kando mwa Ziwa Erhai, mamia ya maili kutoka nyumbani kwao Mkoani Yunnan, kusini-magharibi mwa China. Tarehe hiyo ya Mei 20 ina umuhimu maalumu nchini China, kwani namna yake ya kuitamka kwa lugha ya Kichina "520" inafanana na maneno "wo ai ni," yaani "Ninakupenda." Ni wakati wa kilele cha kuandikisha ndoa, ukishuhudia mistari mirefu katika sehemu za kuandikisha ndoa kote nchini humo.
Huku China ikiwa imeondoa kizuizi cha kutoka kwenye makazi yaliyosajiliwa wakati wa kuandikisha ndoa mapema mwezi huu, wanandoa wanakumbatia mtindo mpya wa "harusi pamoja na safari ya kutalii", wakiunganisha ndoa na likizo zao za mapumziko.
"Kwa kuwa kuandikisha ndoa kumekuwa rahisi sana, tumeamua kufunga ndoa mahali ambapo tulikutana kwa mara ya kwanza," amesema Yang, kutoka Kunming, mji mkuu wa mkoa wa Yunnan. Sehemu ya kuandikisha ndoa unapatikana kwenye peninsula kwenye Ziwa Erhai, ambapo sherehe ya harusi za makundi ilifanyika Jumanne asubuhi katika Eneo linalojiendesha la Kabila la Wabai la Dali, pia mkoani humo Yunnan.
Yang ameongeza kuwa kufuatia sherehe ya harusi, wanandoa hao watatumia siku chache mjini Dali kama sehemu ya fungate.
Sheria mpya ya China ya kuondoa vizuizi vya kuandikisha ndoa imefanya kuandikisha ndoa katika maeneo mbalimbali kuwa rahisi zaidi, hasa kwa wale wanaofanya kazi nje ya makazi yao.
Kwa mujibu wa sensa ya taifa ya China mwaka 2020, idadi ya watu wanaohama kuishi maeneo mengine mbali na walikozaliwa nchini China ilifikia milioni 376, wakiwemo wahamiaji milioni 125 wa kati ya mikoa mbalimbali.
Kwa vile sera hiyo haihitaji tena watu kujiandikisha ndoa zao kutoka makazi yaliyosajiliwa, wanandoa vijana wanapendelea kupanga harusi zao kwa namna yao wenyewe -- kusafiri hadi mahali pazuri kwa ajili ya harusi ya ukumbusho, au harusi za safari.
Ili kuvutia wanandoa zaidi kupanga harusi zao huko kukuza uchumi wa matumizi, maeneo kote nchini China yamekuwa yakichukua hatua mbalimbali.
Kwa mfano, Chengdu, mji mkuu wa Mkoa wa Sichuan, umehamishia sehemu ya kuandikisha ndoa kwenye kilele cha mlima chenye theluji kwenye mwinuko wa mita 3,250 kwa ajili ya huduma za kuandikisha ndoa, mahali pa juu kabisa katika mji huo.
Chen Liuling, mpiga picha wa kibinafsi wa Chengdu, amesema upigaji picha wakati wa kuandikisha ndoa kwa kawaida bei yake ni kuanzia yuan 200 (kama dola za Kimarekani 27.8) hadi yuan 400, huku studio za hali ya juu hutoza hadi yuan 699.
"Wanandoa wengi wanatafuta hisia za sherehe na gharama nafuu. Wako tayari kutumia yuan mia chache kuhifadhi kumbukumbu ya wakati huu maalum," amesema.
Zhao Canhui, mkuu wa tawi la harusi za safari la jumuiya ya utalii ya Dali, amesema kuwa vijana leo wana tafsiri tofauti zaidi za mapenzi, ikisababisha kuibuka kwa harusi za kusafiri kwenye vivutio.
Amesema kuwa miundo hiyo ya kuandikisha ndoa yenye uvumbuzi inaonyesha kuinua kwa kiwango cha matumizi kufuatia kuondoa vizuizi vya kuandikisha ndoa na pia tafsiri mpya za vijana kwa sherehe za harusi, ikifanya "uchumi mtamu" kuwa injini mpya ya ukuaji.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma