

Lugha Nyingine
Waziri wa fedha wa Afrika Kusini awasilisha upya bajeti ya 2025 bila kuongeza VAT (3)
![]() |
Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini, Enoch Godongwana akitoa hotuba yake ya bajeti ya 2025 mjini Cape Town, Afrika Kusini, Mei 21, 2025. (Picha na Xabiso Mkhabela/Xinhua) |
CAPE TOWN - Waziri wa Fedha wa Afrika Kusini Enoch Godongwana amewasilisha tena Bajeti ya mwaka 2025 mbele ya bunge jana Jumatano, bila kujumuisha ongezeko la kodi ya VAT na kuweka kipaumbele kwa matumizi ya kijamii na ukuaji wa uchumi huku akilenga kudhibiti deni la umma.
Hayo yanajiri baada ya bajeti hiyo kucheleweshwa kutoka tarehe yake ya awali ya Februari kutokana na mivutano ya ndani kuhusu mapendekezo ya ongezeko la VAT.
Machi 12, Godongwana aliwasilisha mapitio ya bajeti iliyopendekeza kuongeza VAT asilimia 0.5 mwaka 2025/26 na nyingine 0.5 mwaka 2026/27, na kupandisha kiwango cha VAT hadi asilimia 16 ifikapo mwaka wa fedha 2026/27.
Akitoa toleo lake la tatu la hotuba ya bajeti ya 2025 kwenye kikao cha Bunge la Kitaifa jana Jumatano alasiri, waziri huyo wa fedha ameelezea mambo kadhaa muhimu yaliyorekebishwa katika bajeti hiyo, ikiwa ni pamoja na hali ya uchumi wa nchi, makadirio ya ukuaji, gharama kubwa za kulipa deni, kuondoa ongezeko la VAT lenye utata, na kuendelea kutoa ruzuku ya misaada ya kijamii.
"Sasa tuna udhahiri: VAT itaendelea kuwa asilimia 15. Uamuzi huu unaonyesha dhamira yetu ya kuwasikiliza Waafrika Kusini na vyama vyote vya kisiasa vinavyowakilishwa katika Bunge hili," amesema.
Hata hivyo, ili kuwianisha athari ya kuondoa ongezeko hilo la VAT, Godongwana amesema ushuru wa mafuta utarekebishwa kwa mfumuko wa bei.
Amebainisha kuwa uchumi wa Afrika Kusini huenda utaongezeka kwa asilimia 1.4 mwaka huu, chini ya asilimia 1.9 iliyotarajiwa Machi, na kisha kupanda hadi asilimia 1.6 mwaka 2026 na asilimia 1.8 mwaka 2027.
Katika hotuba yake hiyo, Godongwana amesema bajeti hiyo bado inalenga kukuza pato la nchi kwa haraka zaidi kuliko matumizi yake, huku deni la Serikali likitarajiwa kuchukua asilimia 77.4 ya pato la taifa, kutoka asilimia 76.2 iliyotarajiwa Machi.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma