

Lugha Nyingine
Bidhaa zenye umaalumu zaonyesha uwazi na kufungua uwezo wa kibiashara kati ya China na CEEC
NINGBO – Yakiwa na bidhaa zaidi ya 8,000 zinazoonyeshwa, kuanzia bidhaa za jadi kama vile mvinyo na jibini hadi aina za kisasa kama vile miwani ya VR, Maonyesho ya 4 ya China na nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki CEEC na Maonyesho ya Kimataifa ya Bidhaa za Matumizi yamefungua pazia lake mjini Ningbo, Mkoani Zhejiang, mashariki mwa China jana Alhamisi, yakifungua uwezekano mkubwa wa ushirikiano kati ya China na Nchi za CEEC.
Kwa mujibu wa waandaaji, maonyesho hayo yanayofanyika kuanzia Alhamisi hadi Jumapili wiki hii, yamevutia kampuni 435 kutoka nchi 14 za CEEC na nchi nyingine tisa, zikiwemo Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia.
Waandaaji hao wamesema, kampuni jumla ya 1,028 za China pia zinashiriki kwenye maonyesho hayo, zikionyesha viwanda vyenye umaalumu za nchini humo na bidhaa za matumizi zenye ushindani. Wameeleza kuwa, pia yanavutia wanunuzi zaidi ya 3,000 kutoka nchi na maeneo 72.
Taarifa iliyotolewa na waandaaji hao inaonesha kuwa, makubaliano ya kuagiza bidhaa yenye thamani ya yuan zaidi ya bilioni 10 (dola za Kimarekani kama bilioni 1.39) yanatarajiwa kufikiwa na washirika wa CEEC kwenye maonyesho hayo.
Waandaaji wamefafanua kuwa, licha ya bidhaa hizo za jadi za matumizi, maonyesho hayo pia yanaonyesha teknolojia za kidijitali na za akili bandia, yakitumika kama jukwaa pana la kuwasilisha mafanikio ya uvumbuzi katika sekta kama vile ndege, vyombo vya VR, vifaa vya matibabu na roboti zenye muundo wa binadamu.
"Maonyesho haya ni lango la bidhaa zetu kufikia masoko ya kimataifa, na tunapanga kuanzisha makao makuu katika eneo la CEEC ili kuangaza zaidi na kupanua uwepo wetu katika kanda hiyo," amesema Fan Rui, mwanzilishi wa Kampuni ya Kiteknolojia ya Aoxue Ruishi, ambaye ameleta miwani ya uhalisia ulioongezwa (XR) ya kampuni yake kwenye maonyesho hayo.
Yakiwa yanaandaliwa kwa ushirikiano wa serikali ya mkoa wa Zhejiang na Wizara ya Biashara ya China, Maonyesho hayo, yaliyoanzishwa rasmi mwaka 2019, yametoa mchango muhimu katika kuongeza mauzo ya bidhaa za nchi za CEEC kwenye soko la China, na kuimarisha mapatano ya ushirikiano kati ya China na nchi za CEEC.
Takwimu kutoka wizara ya biashara ya China zinaonyesha kuwa mwaka 2024, thamani ya biashara kati ya China na nchi hizo za CEEC iliongezeka kwa asilimia 6.3 mwaka hadi mwaka, ikifikia rekodi ya juu ya dola za Marekani bilioni 142.3.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma