

Lugha Nyingine
Maonyesho ya biashara ya eneo la Magharibi ya China yashuhudia makubaliano yenye thamani ya yuan zaidi ya bilioni 200 yakitiwa saini
CHONGQING - Maonyesho ya 7 ya Kimataifa ya Uwekezaji na Biashara ya Eneo la Magharibi ya China yameanza rasmi jana Alhamisi katika Mji wa Chongqing, kusini-magharibi mwa China huku makubaliano ya mradi yaliyosainiwa ana kwa ana kwenye maonyesho hayo yakiwa na thamani yenye kuzidi Yuan bilioni 200 (dola za Kimarekani takriban bilioni 27.8).
Waandaji wa Maonyesho hayo, wameialika Thailand kuwa nchi mgeni wa heshima, Mkoa wa Sichuan kuwa mkoa mgeni wa kudumu, na Mkoa wa Utawala Maalum wa Hong Kong kuwa mji mpya mgeni ulioongezwa.
Maonyesho hayo yamevutia kampuni za kiviwanda zaidi ya 1,300 kutoka nchi na maeneo 39, zikiwemo kampuni za kiviwanda 56 za serikali kuu ya China, kampuni 47 miongoni mwa Kampuni Bora 500 Duniani, kampuni 93 za kimataifa, na kampuni ongozi binafsi 286.
Kwa mujibu wa kamati ya maandalizi, sekta za viwanda na huduma za kisasa zimechukua zaidi ya asilimia 75 ya miradi yote iliyotiwa saini, ikijumuisha sekta kama vile anga ya juu, nyenzo za teknolojia ya hali ya juu, nishati na vifaa vya teknolojia ya kisasa.
Shughuli za kiutamaduni zafanyika kwenye Jukwaa la Russia na China mjini Khabarovsk, Russia
Miti ya jacaranda katika mchanuo wa maua yavutia watalii mjini Kunming, China
Upandaji mahindi waingia kipindi cha kilele katika Mkoa wa Mongolia ya Ndani, China
UNESCO latoa wito upya wa kuimarishwa ulinzi wa maeneo ya urithi ya Afrika
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma