Trump amkabili Rais wa Afrika Kusini kwa kutumia madai ya nadharia za njama

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 23, 2025
Trump amkabili Rais wa Afrika Kusini kwa kutumia madai ya nadharia za njama
Rais wa Marekani, Donald Trump (Kulia) akikaribisha Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini(katikati) kwenye Ikulu ya White House mjini Washington, D.C., Marekani, Mei 21, 2025. (Xinhua/Hu Yousong)

SACRAMENTO, Marekani - Rais Donald Trump wa Marekani amemkabili Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa juzi Jumatano kwa kutumia nadharia za njama juu ya "mauaji ya kimbari dhidi ya watu weupe" nchini Afrika Kusini, ambayo Rais Ramaphosa ameyakanusha vikali, ambapo kwenye mkutano wao katika Ofisi ya Oval, Trump ameishutumu Afrika Kusini kwa "mauaji ya kimbari dhidi ya weupe" na kutwaa ardhi bila haki, na kisha bila kutarajia akawasilisha video na karatasi za habari zilizochapishwa ambazo amedai zinathibitisha madai yake hayo.

Ramaphosa, ambaye aliwasili Washington kwa matumaini ya kuboreshwa kwa mambo ya biashara na kupunguza mvutano kati ya pande mbili, amepinga hoja hizo za Trump kwenye mkutano huo huku akipinga dhana kwamba Waafrika Kusini weupe wanaikimbia nchi hiyo kutokana na sera za kibaguzi akisema kuwa kuna uhalifu nchini Afrika Kusini na wengi wa waathirika ni watu Weusi.

Vyombo vya habari vilishtushwa na kitendo hicho kisicha cha adabu cha Trump, vikisema sehemu kubwa ya habari alizotumia kwenye mkutano huo kujaribu kuthibitisha kuwa "mauaji ya kimbari dhidi ya weupe" yanatokea Afrika Kusini "zimekuwa zikikanushwa mara kwa mara."

"Kati ya orodha ya kutakatisha nadharia hizo za njama iliyotolewa kwenye mkutano huo wa Trump na Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini leo (juzi Jumatano), karibu kila kitu kimekanushwa. Baadhi ya Waafrika Kusini wamesema kwamba wanaamini kwamba habari hizo ni 'propaganda za AfriForum' -- kundi la Waafrikana-Weupe linalokosolewa kuwa ni kundi la Weupe," shirika la habari la CNN limeripoti.

Mvutano huo umekuja wakati ambapo uhusiano kati ya nchi hizo mbili umekuwa mbaya, ambapo tangu Ramaphosa atie saini Muswada wa Kutwaa Ardhi na kuwa sheria mwezi Januari, Trump amekuwa akikosoa sheria hiyo ya mageuzi ya ardhi kwa "kuwabagua" watu weupe wa nchi hiyo.

Katika miezi ya hivi karibuni, Trump amekuwa akiikosoa Afrika Kusini mara kwa mara, hasa kwa kufuta ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kukabiliana na UKIMWI na kudai kwamba "mauaji ya halaiki" dhidi ya Waafrika Kusini weupe yanaendelea, madai ambayo yamekanushwa na serikali ya Afrika Kusini.

Mwezi Machi, Marekani ilimfukuza Balozi wa Afrika Kusini wakati huo Ebrahim Rasool, ikidhoofisha zaidi uhusiano wao. Kufukuzwa huko kulikuja baada ya Rasool kuhutubia mkutano wa mtandaoni ulioandaliwa na Taasisi ya Mapungubwe ya Tafakuri ya Kimkakati, akitoa maoni yake juu ya utawala wa Trump.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio awali alisema Jumanne kwamba Trump hatashiriki katika mkutano ujao wa viongozi wa Kundi la 20 (G20) nchini Afrika Kusini baadaye mwaka huu.

Afrika Kusini imekuwa ikikanusha na kupinga vikali shutuma hizo kutoka utawala wa Trump, ikisema amri tendaji ya kuzuia misaada "inakosa msingi wa ukweli halisi na inashindwa kutambua historia ya kina na chungu ya Afrika Kusini ya ukoloni na ubaguzi wa rangi."

(Wahariri wa tovuti:Zhou Linjia,Zhao Jian)

Picha